BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
KITUO cha Luninga cha Agape Television Network (ATN) kimepata haki ya kuonesha moja kwa moja mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya timu ya Yanga na Azam FC utakaofanyika kesho kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 alasiri.

Mkurugenzi wa michezo wa ATN Denis Msemwa alisema wamejipanga kurusha mchezo huo ambao utakuwa na muonekano bora yaani HD huku matukio yote muhimu yakionekana.

Aidha Msemwa alisema pia vyombo vyengine vya habari vitaruhusiwa kurekodi dakika 15 za mwanzo na 15 za mwisho ili kuweza kutumia katika taarifa za habari ila baada ya mchezo wanaweza kupata CD ya mechi nzima.

Kwa upande wake Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema endapo mchezaji ataonywa kwa kadi katika mchezo huo adhabu hiyo itaendelea hadi kwenye mechi za ligi kuu kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu ya Vodacom.

"Kama mnakumbuka mchezaji Erasto Nyoni alioneshwa kadi ya njano katika mchezo kama huu mwaka jana ikaigharimu Azam hadi kupokwa alama kwahiyo wachezaji wanatakiwa wawe makini," alisema Lucas.

Viingilio katika mchezo huo ni VIP A 20000 VIP B na C 15000 huku mzunguko  ukiwa ni 5000.

Post a Comment

 
Top