BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Bunju
WAJUMBE wa kamati ya Utendaji ya klabu ya Simba wakiongozwa na Rais Evans Aveva, leo wametembelea Bunju ambako ujenzi wa uwanja wa timu hiyo unaendelea kwa kasi.

Ujenzi huo ambao ulianza takribani wiki mbili zilizopita umefikia hatua nzuri ambapo kifusi kimeshamwagwa hivyo kusubiri kusawazishwa ili hatua ya kuweka nyasi bandia ianze.

Safari ya wajumbe hao ipo kwenye ratiba ya 'Simba Week' ambayo inafikia kileleni kesho ambapo timu itapambana na AFC Leopards ya Kenya katika dimba la Taifa.


Akizungumza na viongozi wa matawi na wanachama wachache waliohudhuria Aveva alisema kuna uwezekano mkubwa uwanja huo ukaanza kutumika mwishoni mwa mwezi Septemba.

"Kinachosubiriwa hapa ni nyasi kutolewa bandarini, tukishalipa kodi tukazitoa basi ni kumuita mtaalamu kutoka China aje kuanza kazi yake, naamini mwishoni mwa Septemba vijana wanaweza kuanza kufanya mazoezi hapa," alisema Aveva.

Ujenzi wa uwanja huo ni moja ya ahadi za Aveva alipokuwa anatangaza sera zake ili achaguliwe kuwa Rais wa kwanza wa klabu hiyo.

Post a Comment

 
Top