BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
RAIS wa klabu ya Simba Evans Aveva anashikiliwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU kwa ajili ya uchunguzi baada ya tuhuma ambazo hazikuwekwa wazi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni Evalist Foime alisema Rais huyo ameshikiliwa katika kituo cha Polisi Urafiki huku uchunguzi ukiendelea kabla ya hatua za kisheria kufuatwa.

Kwa upande wake Msemaji wa TAKUKURU Musa Misalaba amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwa wapole kipindi hiki ambacho Rais wao yupo katika uchunguzi kabla ya sheria kufuata mkondo wake.

"Yupo kwenye mikono salama uchunguzi unaendelea kabla ya hatua za kisheria kufuatwa," alisema Misalaba.

Tukio hilo limesababisha sintofahamu miongoni mwa wanachama na wapenzi wa Simba ambao wanaelekea kuadhimisha miaka 80 ya klabu hiyo Agosti 8 (Simba Day).

Post a Comment

 
Top