BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
RAIS wa klabu ya Simba Evans Aveva pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji waliokuwa wakihojiwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU  wameachiwa muda huu kwa dhamana huku wakitakiwa kuripoti tena kesho.

Viongozi hao wanahojiwa kwa tuhuma zinazosemekana kuwa ni rushwa na ukwepaji wa kodi baada ya kile kilichoelezwa kuwa fedha za mauzo ya mchezaji Emanuel Okwi ziliwekwa kwenye akaunti binafsi ya Aveva badala ya ile ya Simba kwa lengo la kukwepa kulipa deni la mamlaka ya mapato TRA.

Aveva alikuwa wa kwanza kukamatwa huku viongozi wengine wakipigiwa simu ili wafike ofisini hapo kwa ajili ya mahojiano ambayo yataendelea kesho.

Mbali na Aveva viongozi wengine walioitwa ili kuhojiwa ni pamoja na makamu wa Rais Geoffrey Nyange 'Kaburu', Kassim Dewji, Said Tully, Jasmin na mhasibu Amosi.

Hata hivyo Jasmine hakuhojiwa kwahiyo atalazimika kufika ofisini hapo kesho ambapo pia Amosi amepewa melekezo ya kuripoti saa 4  asubuhi huku Aveva yeye akitakiwa kufika saa 7 mchana. 

Shauri hilo linasimamiwa na mwanasheria wa Simba Evodius Mtawala ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa wekundu hao.

Post a Comment

 
Top