BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Dar
BAADA ya kusambaa kwa picha mtandaoni zikimuonesha mshambuliaji wa Azam Kipre Tchetche akitambulishwa na klabu ya Al Nahdha ya Oman Uongozi wa klabu hiyo hawatambui chochote kinachoendelea.

Mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast alikuwa akihusishwa na kujiunga na kujiunga na moja ya klabu kongwe hapa nchini kabla ya kuibukia nchini Oman.

Mtendaji mkuu wa Azam Saad Kawemba ameiambia BOIPLUS kuwa hawafahamu chochote kuhusu kuondoka kwa mshambuliaji hiyo kwakua bado amebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja ndani ya wanalambalamba hao.

"Kipre bado ni mchezaji wetu halali ana mkataba wa mwaka mmoja kama kuna timu inamuhitaji lazima waje kwetu tukae nao tumalizane," alisema Kawemba.

Aidha Mtendaji huyo alisema iwapo utaratibu wa kusajiliwa hautofuatwa Azam hawatatoa nyaraka zozote kwa mshambuliaji huyo kitu kitakochosababisha kutocheza katika timu yoyote.

"Hatutatoa nyaraka mpaka utaratibu utakapofuatwa vinginevyo hatocheza huko aliko," alisema Kawemba.

Tangu kumalizika kwa msimu wa ligi wachezaji wa Azam walipopewa likizo Kipre hakurudi tena Azam huku wengine wote wakifanya mazoezi chini ya kocha Mhispania Zeben Hernandez.

Post a Comment

 
Top