BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, umefanyia kazi maombi ya wapenzi wa soka nchini, walioomba mchezo wao wa kirafiki dhidi ya URA ya Uganda kesho Ijumaa ufanyike usiku badala ya jioni kutokana na siku hiyo kuwa ya kazi.

Katika marekebisho waliyofanya kuhusiana na mchezo huo, sasa utafanyika Uwanja wa Azam Complex kesho Ijumaa saa 1.00 jioni badala ya saa 10.00  muda uliopangwa awali, kwa viingilio vilevile vya Sh. 1,000 kwa viti vya kawaida na 3,000 kwa viti maalumu (V.I.P).

Azam FC inapenda kuwakaribisha mashabiki wote wa soka kuhudhuria mchezo huo unaotarajia kuwa mkali na wa aina yake utakaopambwa na burudani safi kutokana na ubora wa vikosi vyote viwili vinavyocheza soka la kitabuni.

Post a Comment

 
Top