BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
TIMU ya Azam FC imefuta uteja kwa Yanga baada ya kuibuka mabingwa wapya wa Ngao ya Jamii kwa mikwaju ya penalti 4-1 katika mchezo wa ngao ya Jamii unaoshiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu hizo zilitoka sare ya kufungana magoli 2-2 katika muda wa kawaida kabla ya kwenda kwenye changamoto ya mikwaju ya penalti na Azam kuibuka na ushindi huo.

Yanga walicheza vizuri kipindi cha kwanza ambapo Donald Ngoma alifunga magoli yote mawili ndani ya dakika mbili kutokana na umakini mbovu wa mabeki wa Azam huku timu nzima ikicheza bila maelewanao mazuri.

Kipindi cha pili Azam walikuja juu na kuwashambulia sana Yanga ambapo dakika ya 69 beki Shomari kapombe alifunga goli baada ya mabeki wa Yanga kushindwa kuondoa mpira katika lango lao kabla ya John Bocco kuongeza  la pili kwa mkwaju wa penalti kufuatia Hajji Mwinyi kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Katika mchezo huu safu za kiungo za timu zote mbili zilifanya kazi ya ziada kuonesha umahiri wa kuzuia na kupandisha mashambulizi hali iliyopelekea kuongeza ladha ya mchezo.

Wachezaji waliofunga penati kwa upande wa Azam ni Bocco,Himid Mao,Kapombe na Michael Boloue huku Yanga akifunga Dida pekee. Waliokosa penati kwa Yanga ni Hassan Kessy na Haruna Niyonzima.

Katika michezo mitatu mfululizo ya ngao ya Jamii Yanga imeshinda yote huku huu wa leo ndo Azam wameibuka na ushindi.

Post a Comment

 
Top