BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Chamazi
TIMU  ya Azam FC imelazimishwa sare na watoza ushuru wa Uganda klabu ya URA ya goli 1-1 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi usiku huu.

Azam walionekana kuzidiwa karibia kila Idara hususani kipindi cha kwanza baada ya wachezaji wake kukosa umakini na kupoteza mipira mingi.

Mshambuliaji Bogota Labama aliipatia URA goli la kuongoza dakika 46 kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya eneo la hatari baada ya Michael Boloue kucheza rafu.

Nahodha John Bocco aliyetokea benchi aliisawazishia Azam kwa mkwaju wa penalti dakika ya 73 baada ya mchezaji mmoja wa URA kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

URA itashuka tena dimbani siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa kumenyana na Simba katika mchezo wa kujipima nguvu ili kujiandaa na ligi.

Post a Comment

 
Top