BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu , Dar
TIMU ya Azam  imeibuka na ushindi wa Mabao 3 -0 dhidi ya Majimaji katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye uwanja Azam Complex ulioko Chamazi nje kidogo ya  jijini la Dar es Salaam.

Azam walianza mchezo huo kwa kasi ambapo dakika ya pili mshambuliaji John Bocco aliipatia timu yake bao baada ya kupata krosi maridhawa ya Shomari Kapombe.

Bao hilo lilidumu hadi timu hizo zikienda mapumziko. Kipindi cha pili Azam walianza mchezo kwa kasi na kuonekana wakihitaji alama tatu ambapo Mudathiri Yahya aliwafungia wenyeji bao la pili dakika ya 68 .

Wakati mashabiki wa Azam FC wakifurahi mabao hayo mawili Nahodha Bocco alihitimisha karamu ya magoli kwa shuti kali lililotinga wavuni moja kwa moja.

MATOKEO MENGINE YA MECHI ZILIZOCHEZWA LEO 

Mbao 0 Vs Mwadui 1

Tz Prison 1 Vs Ruvu Shooting 1

Stand United 0 Vs  Kagera 0

JKT Ruvu 0 Vs Simba 0

Mtibwa 2 Vs Ndanda 1
            
      MECHI ZA KESHO

Yanga vs African Lyon

Toto African vs Mbeya city

Post a Comment

 
Top