BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda
Emery Nimubona (wa kwanza kulia waliochuchumaa) akiwa na kikosi cha Vital'O hivi karibuni.

BAADA ya wekundu wa Msimbazi Simba kukamilisha uhamisho wa straika Laudit Mavugo kutoka Vital'O, mabingwa hao wa Burundi wameamua kujipoza kwa kumsainisha Emery Nimubona aliyechwa na Simba msimu uliopita.

Akizungumza na BOIPLUS kutoka Burundi, Nimubona alisema amesaini mkataba wa miaka miwili na Vital'O lakini yuko huru kuondoka muda wowote akipata timu nyingine inayomhitaji.


"Nimeshajiunga na timu, msimu ujao nitakuwa hapa ingawa tumekubaliana ikitokea timu inahitaji basi wataniruhusu kuondoka, hata Tanzania naweza kurejea," alisema Nimubona.

Mlinzi huyo wa kulia alishindwa kulishawishi benchi la ufundi la Simba hali iliyopelekea uongozi wa klabu hiyo uamue kukubaliananae kuvunja mkataba na akarejea nchini kwao kabla hajarudi tena nchini mwezi uliopita kusaka timu ya kuchezea.

Post a Comment

 
Top