BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
BEKI wa kulia wa Simba aliyesajiliwa msimu huu akitokea Coastal Union, Hamad Juma asubuhi ya leo amepata ajali ya kuanguka bafuni nyumbani kwake kupelekea kuchanika kisogoni.

Msemaji wa Simba Haji Manara aliithibitishia BOIPLUS juu ya tukio hilo akiwa njiani kuelekea Hospitali ya Mwananyamala alikolazwa nyota huyo akipatiwa matibabu.

"Ni kweli Hamad ameanguka na amepoteza damu nyingi sana, sasahivi nipo njiani naelekea Mwananyamala nitakujuza hali yake anavyoendelea," alisema Manara.

Madaktari wamelazimika kumuongezea damu beki huyo ambaye kama hali hiyo itamfanya akae nje kwa muda mrefu basi klabu hiyo itabaki na walinzi wawili wa kulia ambao ni Malika Ndeule mkongomani Janvier Bukungu.

Wakati huo huo wanasimba wameombwa kufika hospitalini hapo kumjulia hali ikiwa ni pamoja na kujitolea damu kwa ajili Hamad na wagonjwa wengine wenye mahitaji ya damu.

Post a Comment

 
Top