BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar
BAADA ya kuanguka bafuni na kupata marejeraha sehemu ya nyuma ya kichwa beki wa Simba Hamad Juma atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili.

Hamad alipata majeraha hayo baada ya kuanguka alipokuwa bafuni akioga Agosti 21 siku moja baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Ndanda FC uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Daktari wa klabu hiyo Yassin Gembe ameiambia BOIPLUS kuwa beki huyo anaendelea vizuri na baada ya wiki mbili mchezaji huyo wa zamani wa Costal Union atarejea dimbani.

"Anaendele vizuri na jeraha lake linaendelea kupona, tunategemea ndani ya wiki mbili atakuwa amepona na kurejea uwanjani," alisema Gembe.

Aidha Gembe alisema tofauti na Hamad hakuna mchezaji mwingine ambaye ni majeruhi kwahiyo kocha Joseph Omog ana wigo mpana wa kuchagua kikosi katika michezo ya ligi.

Simba itashuka dimbani Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kumenyana na JKT Ruvu katika muendelezo wa ligi baada ya wiki iliyopita kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Ndanda.

Post a Comment

 
Top