BOIPLUS SPORTS BLOG

LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI Christian Benteke atafanyiwa vipimo vya afya leo hii baada ya kukubaliana  kujiunga na Crystal Palace akitokea Liverpool.

Palace wamekubali kutoa dau la pauni  32 milioni kwa majogoo hao wa  jiji kwa ajili ya  Benteke ambaye ameshindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Jurgen Kloop.

 Palace wako tayari kumfanya  Benteke kuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa gharama kubwa katika historia ya klabu hiyo inayonolewa na kocha Alan Pardew .

Liverpool walilipa pauni 32.5 milioni kwa Aston Villa  mwaka jana lakini alishindwa kuendana na falsafa ya  Klopp.

Pardew anamchukua raia huyo wa Ubelgiji baada ya kuondokewa na washambuliaji  Emmanuel Adebayor, Dwight Gayle and Marouane Chamakh huku akiwa na pesa za kutosha baada ya kumuuza   Yannick Bolasie kwenda Everton kwa ada ya pauni 28 milioni.

Klopp hakumjumuisha mshambuliaji huyo katika kikosi kilichoshinda magoli 4-3 dhidi ya Arsenal Jumapili iliyopita katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Uingereza licha ya Daniel Sturridge kuwa majeruhi.

Post a Comment

 
Top