BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Dar
KUELEKEA mchezo wa ngao ya Jamii dhidi Yanga timu ya Azam FC imejipanga kuibuka na ushindi katika mchezo huo utakaofanyika kesho uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo unaashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu ya Vodacom ambapo wikiendi ijayo nyasi za viwanja mbali mbali zitakuwa katika wakati mgumu.

Nahodha wa timu hiyo John Bocco 'Adebayor' ameiambia BOIPLUS kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwakua timu zote zimejipanga  vizuri huku wakiwa na wachezaji wenye uwezo wa kubadili matokeo muda wowote lakini mwisho wa kuonewa na Yanga umewadia.

"Mchezo ni mgumu ila sisi tumejipanga vizuri, wachezaji tuna morali na tumepanga kufuta uteja kwa Yanga," alisema Bocco.

Kwa upande wake msemaji wa klabu hiyo Jaffar Iddi alisema maandalizi yote yamekamilika na wachezaji wamepata kila kitu walichokuwa wakihitaji tayari kwa mtanange huo.

Azam pia watautumia mchezo huo kuwatambulisha wachezaji wao wapya waliowasajili katika msimu huu ambao unatabiriwa kuwa mgumu kwa timu zote.

Post a Comment

 
Top