BOIPLUS SPORTS BLOG

LONDON, Uingereza
VIJANA wa kocha Antonio Conte, Chelsea leo wameianza vyema michuano ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Wagonga nyundo Westham.

Eden Hazard aliwaamsha mashabiki 41,000 waliohudhuria katika dimba la Stamford Bridge kwa bao safi la penati dakika ya 47 kabla James Collins hajaisawazishia Westham dakika 30 baadae.


Ikiwa imesalia dakika moja tu mwamuzi AnthonyTaylor amalize mtanange huo, Diego Costa aliwapatia Chelsea bao la ushindi na kuzima kabisa ndoto za vijana wa kocha Slaven Bilic kuambulia japo pointi moja.

Mchezo huo ulitawaliwa na undava ambapo jumla ya kadi za njano saba zilionyeshwa. Kwa upande wa Chelsea Ngolo Kante, Costa, Azpilicueta, Nemanja Matic na Pedro Rodrigues walilimwa kadi za njano huku Collins na Antonio wakipewa kwa upande wa Westham.

Post a Comment

 
Top