BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
BEKI wa kati wa timu ya Simba Novaty Lufunga aliyepata majeraha kwenye mchezo wa ligi uliomalizika kwa sare ya kutofungana dhidi ya JKT Ruvu amepona na kesho ataanza mazoezi na wenzie.

Lufunga ambaye ameanza kuaminiwa na kocha Joseph Omog baada ya kuanza mechi zote hata zile za kujipima nguvu sambamba na beki raia wa Zimbabwe Method Mwanjale, amerejesha imani ya safu ya ulinzi ya Simba ambayo msimu uliopita haikuwa vizuri.

Daktari wa timu hiyo Yassini Gembe ameiambia BOIPLUS kuwa beki huyo aliumia mkono baada ya kuuangukia lakini anaendelea vizuri ambapo kesho ataanza mazoezi pamoja na wenzake.

"Anaendelea vizuri na kesho ataanza mazoezi alikuwa amepata maumivu kwenye mkono wake lakini tunamshukuru Mungu yuko poa kwa sasa," alisema Gembe.

Simba ina mabeki wanne wazuri wa kati ambao ni Lufunga, Mwanjale,Juuko Murshid pamoja na Emmanuel Semwanza huku wote wakipigania kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Omog.

Safu hiyo imeruhusu goli moja pekee kwenye michezo miwili iliyoshuka dimbani tangu kuanza kwa ligi ya Vodacom iliyoanza Agosti 20.

Post a Comment

 
Top