BOIPLUS SPORTS BLOG

CORK, Ireland
TIMU ya KRC Genk inayoshiriki ligi kuu nchini Ubelgiji leo imefanikiwa kusonga hatua moja zaidi mbele kuelekea hatua ya makundi ya michuano ya Europa 2016/17 kwa kuibutua Cork City ya Ireland mabao 2-1.

Alikuwa ni mkali Thomas Buffel aliyewainua vitini mashabiki wachache wa Genk qaliohudhuria mechi hiyo katika uwanja wa Turner's Cross, baada ya kufunga bao safi katika dakika ya 13 tu ya mchezo na kuwashtua wenyewe.

Bao hilo liliwaongezea nguvu Genk ambao katika mchezo wa awali walipata ushindi mwembamba wa bao bao 1-0 kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Cristal Arena. Mlinzi Dawaest akaipatia Genk bao la pili dakika 4 kabla ya mapumziko.

Kipindi cha pili Cork walikuja juh na kutaka kusawazisha mabao hayo ndipo jitihada zao zilizaa matunda katika dakika ya 63 ambapo Alan Bennett aliipatia timu hiyo bao pekee na la kufutia machozi.

Straika mtanzania Mbwana Samatta ambaye ametoka kwenye maumivu ya mgongo, alipumzishwa katika dakika 77 na nafasi yake ikachukuliwa na Bryan Heynen.

Post a Comment

 
Top