BOIPLUS SPORTS BLOG

GENK, Ubelgiji
WAWAKILISHI wa Ubelgiji kwenye hatua ya makundi ligi ya Europa, KRC Genk leo wameibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya ZulteWaregem katika dimba la Cristal Arena ushindi ambao umewasogeza jirani na kilele cha msimamo wa ligi kuu.

Mechi hiyo ya kukata na shoka ilishuhudia ikimaliza dakika 45 za kwanza bila timu yoyote kuziona nyavu za mwenzake huku Genk wakionekana kuwaandama wageni wao bila mafanikio.

Alikuwa ni kiungo mshambuliaji kutoka Hispania, Alejandro Pozuelo ndiye aliyewapatia alama tatu Genk baada ya kuipatia timu hiyo bao pekee katika dakika 80 ambalo lilidumu hadi dakika 90 zinamalizika.

Kwa ushindi huo Genk imefikisha pointi 10 hivyo kukwea hadi nafasi ya tatu ikiwa ni pointi moja nyuma ya Sporting Charleroi wanaoongoza ligi lakini sawa na Waregem inayoshika nafasi ya pili kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Post a Comment

 
Top