BOIPLUS SPORTS BLOG

Ghent, Ubelgiji
BAO la dakika ya 90 lililowekwa nyavuni na Jeremy Perbet lilitosha kuwathibitishia pointi tatu wenyeji KAA Gent katika wa ligi kuu Ubelgiji dhidi ya KRC Genk kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Ubelgiji.

Gent wameibuka na ushindi huko kwa 'mbinde' baada ya kushindwa kuzifumania nyavu za Genk mapema licha ya kufanya mashambulizi kadhaa yaliyoishia kwenye miguu ya walinzi wa Genk.

Mfungaji wa bao hilo pekee lililowapeleka Gent hadi nafasi ya tano baada ya kujikusanyia pointi nne katika mechi mbili, aliingia uwanjani katika dakika ya 82 akichukua nafasi ya Khalifa Coulibaly.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Ghelamco Arena, kadi mbili pekee za njano zilitolewa kwa walinzi wa Genk Sand Walsh na baadaye Dries Wouters aliyeingia kuchukua nafasi ya Walsh.

Straika mtanzania Mbwana Samatta leo alianzia benchi
 hadi katika dakika ya 66 ambapo kocha Peter Maes alimuita nje Nikos Karelis na kumpa nafasi Samatta ambaye hata hivyo hakuweza kuinusuru Genk kupata kipigo.

Baada ya michezo miwili ili ligi hiyo inaongozwa na Anderlecht  ambao wanafanana pointi na Zulte Waregem pamoja na Sporting Charleroi kila moja ikiwa  na pointi sita. Genk wenyewe wamebakia kwenye nafasi ya 10 wakiwa na pointi  tatu tu.

Post a Comment

 
Top