BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
MANCHESTER United imeibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Southampton katika muendelezo wa ligi kuu ya Uingereza mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Old Trafford.

Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic aliwapatia United goli la kuongoza dakika ya 36 baada ya kupokea krosi safi toka kwa Wayne Rooney upande wa kulia wa uwanja baada ya mabeki wa Saints kushindwa kuokoa mpira kwenye eneo lao la hatari.

Mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba alionesha kandanda safi lililowashawishi United kutoa pauni 89 milioni kwa Juventus ili kupata huduma ya kiungo huyo fundi wa mpira ambaye aliongoza kwa kugusa mpira mara nyingi kwenye mchezo huo.

Dakika 51 Ibrahimovic tena alifunga goli la pili kwa mkwaju wa penalti baada ya Luke Shaw kuangushwa na beki  Clasie kwenye eneo la hatari kabla mshambuliaji huyo raia wa Sweden kuweka mpira kimiani.

United sasa wamefikisha alama 6 na wanaongoza ligi kutokana na timu nyingine kutoshuka dimbani leo.

Post a Comment

 
Top