BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
TIMU ya soka ya Ruvu Shooting  imekamilisha usajili wa kiungo wa zamani wa Mwadui FC Jabir Aziz kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kuwatumikia maafande hao katika msimu mpya wa 2016/17.

Jabir pia aliwahi kuichezea timu ya Simba kabla ya kutimkia kwa Wana Lambalamba Azam FC ambako pia hakudumu sana akajiunga na Mwadui ya mkoani Shinyanga.

Wachezaji wengine  wapya waliosajiliwa msimu huu na maafande hao na timu walizotoka kwenye mabano ni   Richard Peter (Mbeya city), Elias Emanuel (Polisi Morogoro), Clidel Loita (Mji Njombe), Chande Magoja na Fuluzuru Maganga wote kutoka Mgambo JKT, Shaibu Nayopa (Oljoro JKT), Abrahaman Musa (JKT Ruvu) na Renatus Kisasa ambaye ni mchezaji huru.

Aidha wachezaji wazamani walioachwa ni Ally Khan, Yahya Tumbo, Chagu Chagula, Juma Mpakala, Rashid Gumbo, Kulwa Mobi, Gidion Seppo na George Osei.

Timu hiyo iko kambini Mabatini ikiendelea na mazoezi ambapo  Agost 1, ilicheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Mbeya city na kupata ushindi wa bao 1-0.

Maafande hao leo watashuka dimbani katika uwanja wa chuo cha Polisi, Dar es salaam kucheza na Polisi Dar es salaam ambapo Jumamosi ijayo itakuwa Mabatini ikipambana na Azam FC.

Post a Comment

 
Top