BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
MSHAMBULIAJI wa timu ya Tanzania Prisons Jeremiah Juma amejipanga kuchukua kiatu cha ufungaji bora msimu huu wa ligi ya Vodacom licha ya kuwepo kwa changamoto toka washambuliaji wengine wanaotabiriwa kufanya vizuri katika kuzifumania nyavu.

Mshambuliaji huyo alifunga mabao 14 msimu uliopita na kuisaidia timu yake kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi kuu chini ya kocha Salum Mayanga aliyejiunga na Mtibwa Sugar.

Akizungumza na BOIPLUS Juma alisema nia yake msimu huu ni kuisaidia timu yake kuwa katika nafasi tatu za juu na kufunga magoli mengi zaidi ili kuibuka mfungaji bora.

 “Nimejipanga vizuri kuisaidia timu yangu, nitashirikiana na wachezaji wenzangu ili kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita" alisema Jeremiah.

Mshambuliaji huyo alisema Kocha  wao mpya Abdul Mingane wanamuelewa haraka kitu kitakachosaidia kufanya vizuri katika ligi msimu huu huku akisifia maandalizi ambayo wanafanya katika kila mchezo. 

Prison waliibuka na ushindi wa goli 1-0 ugenini dhidi ya Majimaji na wikiendi ijayo itashuka kwenye uwanja wa Sokoine kumenyana na Ruvu Shooting.

Post a Comment

 
Top