BOIPLUS SPORTS BLOG

 iSheila Ally
BEKI wa zamani wa Simba, Nasoro Masoud 'Chollo' amepewa cheo cha unahodha katika timu yake mpya ya Mwadui FC baada ya klabu hiyo kuachana na nahodha wao Bakari Kigodeko. 

Chollo ambaye amesajiliwa akitokea Stand United amepewa cheo hicho baada ya makocha wake kuridhishwa na nidhamu yake nje na ndani ya uwanja.

Katibu Mkuu wa Mwadui FC, Ramadhan Kilao alimsifu Chollo kwa kutunza kiwango chake ambapo amecheza soka kwa kipindi kirefu na kudai kuwa amekuwa ni mchezaji anayepambana.

"Makocha walipendekeza Chollo awe nahodha akisaidiana na Idd Mobby. Kiukweli Chollo ana nidhamu ya hali ya juu, mzoefu katika ligi na pia anaweza kuzungumza vizuri na wenzake," alisema Kilao

Chollo aliwahi pia kuwa nahodha wa Simba miaka ya nyuma wakati huo Simba inafundishwa na Abdallah Kibadeni alisaidiana na Jamhuri Kihwelu 'Julio' ambaye ni kocha wa Mwadui.

Chollo alivuliwa unahodha Simba wakati huo inafundishwa na Mzambia Patrick Phiri baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Post a Comment

 
Top