BOIPLUS SPORTS BLOG

Swabri Kachwamba
TIMU ya Kagera Sugar 'Wanankulukumbi' imepata mapokezi makubwa mkoani Shinyanga baada kufanya mazoezi katika uwanja wa Kambarage jioni ya  leo.

Kagera itacheza mechi ya kirafiki na Mwadui FC kabla ya kusafiri hadi jijini Mwanza kujipima nguvu na Toto African kwa ajili yakujiweka sawa kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi Agosti 20.

BOIPLUS ilifanya mahojiano  na baadhi ya mashabiki waliojaa katika uwanja huo ambao wamekiri kuwapenda sana Wanankulumbi hao kuliko timu zao mbili za mkoa huo ambazo ni Stand United na Mwadui FC.

"Unajua msimu uliopita walitumia uwanja huu kama uwanja wao wa wanyumbani na ukatufanya tukawa na timu tatu hapa Shinyanga kwahiyo tunaipenda sana" alisikika mmoja wa mashabiki wa timu hiyo.

"Unajua  watu watatuona wasaliti lakini sisi tunashabikia, na siku zote kizuri chajiuza kibaya chajitembeza  na heshima walioupa mkoa wetu ni ya kipekee walifanya mkoa wetu kuwa na timu tatu za ligi msimu uliopita," alisema shabiki mmoja aliyejitambilisha Kwa jina moja Erick 

Boiplus pia ikamtafuta mchezaji mpya wa klabu huyo Ibrahim Twaha maarufu kama Messi wa Tanga kuzungumzia mapokezi hayo ambaye  alionesha mshangao mkubwa kutokana na mashabiki wa mkoa huo kuwalaki kwa mapenzi makubwa kuliko hata timu zao zinazowakilisha mkoa huo.

"Sikuamini nilichokiona, ama kweli Shinyanga kuna watu wanaipenda Kagera, hii ni mara yangu ya kwanza kuona mashabiki wengi hivi na wanaimba na kushangilia mazoezi yakiendelea hakika haya ni mapokezi makubwa niliyowahi kuyaona," alisema winga mpya wa timu hiyo Ibrahim Twaha 'Messi'.

Post a Comment

 
Top