BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
HATI ya Uhamisho (ITC) ya mshambuliaji mpya wa Simba Laudit Mavugo imewasili nchini na sasa raia huyo wa Burundi ni mali halali ya Wekundu wa Msimbazi.

Mapema wiki hii Katibu mkuu wa Simba Patrick Kahemele alienda nchini Burundi kumalizana na timu ya zamani ya mshambuliaji huyo FC Vital'O kabla ya kurudi na jibu ambalo ni faraja kwa mashabiki wa Simba.

Awali Vital'O walilipeleka jina la mshambuliaji huyo katika Shirikisho la mpira la Burundi kuonesha kuwa walikuwa na mkataba nae na alikuwa katika kikosi kwa ajili ya msimu mpya wa ligi nchini humo.

Katibu mkuu wa Simba  ameiambia BOIPLUS kuwa tayari ITC za wachezaji wote waliowasajili msimu huu zimefika akiwemo ya Mavugo na washazipeleka Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.

"ITC za wachezaji wote wakigeni tuliowasajili tumezipata na tushazipeleka TFF tayari kuanza kuitumikia Simba" alisema Kahemele.

Mavugo anategemewa kuwepo katika kikosi cha Simba kitakachoshuka dimbani kesho kuwakabili Ndanda FC katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya Vodacom itayochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top