BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Dar
BAADA ya kusambaa kwa taarifa kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji ameamua kujiuzulu wadhifa wake huku pia akisitisha mpango wake wa 'kuikodi' klabu hiyo, mtandao wa Salehjembe umeripoti kuwa amekiri kuchoshwa na mambo yanavyokwenda.
 
Kwa mujibu wa mtandao huo Manji hakutaka kukubali au kukataa juu ya taarifa hizo bali alisema amechoka na asingependa kuulizwa zaidi.
 
Kumekuwa na taarifa kwamba Manji ameamua kuachana na wazo lake la kuwekeza Yanga kwa miaka 10 baada ya kuona hata baadhi ya viongozi wa serikali wakimuandama kwa madai wanatumiwa na baadhi ya mamilionea.

Taarifa nyingine zimeelezwa kwamba, wako wanachama wa Yanga ambao wanaona hawatafaidika na maslahi yao binafsi kama Manji atawekeza, hivyo wamekuwa wakipambana kuhakikisha haingii mkataba na kupewa nafasi hiyo kwa kuwa inaweza kuwavuruga.

Awali, kumekuwa na taarifa Manji ameamua kujitoa kwa kuwa kuna juhudi za chini pia zinazohusisha hadi watu wengine wenye mamlaka katika soka ambao wana hofu na uwekezaji wake.
 
BOIPLUS iliwatafuta watu wa karibu wa Manji ambao walithibitisha juu ya uamuzi huo huku wakisema kuna uwezekano mkubwa kesho akaitisha mkutano wa waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza rasmi kuachana na Yanga.

Post a Comment

 
Top