BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda
AKIWA ndio kwanza amemaliza nusu mwaka tu tangu ajiunge na KRC Genk, nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta ameingia kwenye orodha ya wachezaji muhimu zaidi katika kikosi hicho ambao wakikosekana basi inakuwa ngumu kuziba mapengo yao.

Hali hiyo ilithibitika juma lililopita pale straika huyo anayesumbuliwa na maumivu ya mgongo alipolazimishwa kuingia uwanjani wakati timu yake ikipambana na Cork ya Ireland kwenye mchezo wa marudiano michuano ya Europa."Niliwaambia siko vizuri kwavile nina maumivu ya mgongo lakini kocha alitaka nicheze, nikapewa matibabu maalumu ndipo nikacheza, lakini kama ulitazama mechi utakuwa umeona sikuwa sawa," alisema Samatta.

Katika mchezo huo Genk waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 hivyo kuwaondoa Cork kwa jumla ya mabao 3-1 kutokana na ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Ubelgiji.

Katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KAA Gent juzi, kocha Peter Maes alimpanga tena Samatta ingawa safari hii alimuingiza katika kipindi cha pili.Hata hivyo straika huyo wa zamani wa African Lyon na Simba aliiambia BOIPLUS kuwa kwasasa anaendelea vizuri na muda si mrefu atarejea katika kiwango chake.

Post a Comment

 
Top