BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Selestine Mwesigwa amefungua kozi ya siku tano ya ukocha wa 'Fiziki' itayofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Kozi hiyo itajumuisha makocha 27 ambayo ni mara ya kwanza kutolewa na Shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA kwa Tanzania huku ikitegemewa kuwa itaongeza wataalamu katika medani ya Soka.

Mwesigwa ameishukuru FIFA kuwaletea kozi mbali mbali zikiwemo za ukocha, waamuzi na hii ya fiziki ambayo itazalisha makocha bora watakaokuwa msaada mkubwa kwa Taifa na nje ya nchi.

"Nachukua nafasi hii kuipongeza FIFA kwa nafasi hii ya upendeleo kwetu ambayo tutaitumia vizuri kama tulivyoelekezwa ili iwe msaada kwetu. Pia niwaombe makocha watako hitimu watoe elimu kwa wengine wapate kunufaika" alisema Mwesigwa.

Kwa upande wake mkufunzi wa kozi hiyo kutoka FIFA Daktari Pradit Dutta raia wa India alisema amefurahishwa na mapokezi mazuri aliyoyapata toka TFF ambayo yatamuwezesha kufanya kazi zake katika mazingira mazuri.

"Imani yangu kozi hii itakuwa bora na malengo yaliyokusudiwa yatafikiwa endapo kila mmoja atatimiza majukumu yake," alisema Dutta.

Post a Comment

 
Top