BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
BODI ya Ligi  (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imethibitisha kuwa mchezo wa ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga  na JKT Ruvu  uliopangwa kufanyika Jumatano Agosti 31,  kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam umeahirishwa mpaka utakapopangiwa tarehe nyingine.

Mechi hiyo imeondolewa kutokana na timu ya Yanga kuwa na wachezaji wengi kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinachosafiri Agosti 31, asubuhi kwenda Lagos, Nigeria kwa ajili ya mechi ya mchujo ya michuano ya Kombe la Afrika (AFCON Qualifiers) itakayochezwa Septemba 3.

Mabadiliko hayo hayatavuruga ratiba ya mechi zinazofuata za Ligi Kuu ya Vodacom kwa timu husika.

Tayari timu husika zishapata taarifa kuhusu mabadiliko hayo na kuridhia kulingana na hali halisi.

Post a Comment

 
Top