BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kiingilio cha Sh2,000 kwa mzunguko na Sh 5,000 kwa jukwaa kuu wakati timu ya taifa yaTanzania ya vijana wenye umri wachini ya miaka17 dhidi ya Amajimbos ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakofanyika mwakani nchini Madagascar.

Mchezo huo utaoanza saa 9.00 alasiri Jumapili Agosti 21, kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam utachezeshwa na Mwamuzi Noiret Jim Bacari wa Comoro akisaidiwa na Mmadi Faissoil na Said Omar Chebli wakati mezani atakuwa Ali Mohamed Adelaid huku Kamishna wa mchezo huo akiwa Amir Abdi Hassani kutoka Somalia.

Jumamosi iliyopita Agosti 6   Serengeti ilitoka sare ya 1-1 na Afrika Kusini katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto huku vijana hao wakionesha kandanda safi lillilowavutia mashabiki waliohudhuria mtanange huo.

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime maarufu kama Mchawi Mweusi amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo na kuwapa morali vijana kuibuka na ushindi.

Post a Comment

 
Top