BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga Yusuph Manji amebainisha kuwa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF halipendi maendeleo ya mabingwa hao.

Manji ameyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa dharura unaoendelea hapa katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alisema TFF wamekuwa wakiingilia mambo yao hata kama hawana uwezo nayo kikatiba.

"Hata uchaguzi wetu tuliofanya mwezi wa sita walitaka kuusimamia ambapo ni kinyume cha katiba ya Yanga," alisema Manji.

Mwenyekiti huyo pia alisema TFF haitakiwi kumfungia Mkuu wa kitengo cha Habari wa klabu hiyo Jerry Muro kwakua yeye ndiye aliyemtuma na kama nikufungiwa ingefungiwa Yanga iliyomtuma.

"Hawajaleta nakala ya hukumu kwetu kwahiyo Jerry ataendelea kuwa mfanyakazi wa Yanga" alisema Manji.

BOIPLUS itaendelea kukujuza kila kinachoendelea toka hapa ukumbi wa Diamond Jubilee.

Post a Comment

 
Top