BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
STRAIKA Laudit Mavugo wa Vital'O ya Burundi aliyetua jana usiku Dar kumalizana na Simba amesema kilichomleta nchini ni kulipa deni tu kwa wekundu hao wenye moyo wa uvumilivu.

Akizungungumza na BOIPLUS leo Mavugo ambaye alifikia katika Hotel ya Itumbi iliyopo Magomeni alikiri kuwa bado hajasaini kandarasi na wekundu hao lakini haoni kitakachozuia yeye kuvaa jezi yake namba 45 katika kikosi hicho msimu ujao.

"Sikutaka kusaini pale Vital'O kwavile tu nina deni hapa Simba tangu mwaka jana, nimekuja kulipa. Hawa watu wa Simba ni wavumilivu sana, wangeweza kunishtaki lakini  hawakufanya hivyo, waambie watulie nimekuja kuwafanyia kazi," alisema Mavugo.


Mavugo alikwenda kufanya majaribio katika klabu ya Tours ya Ufaransa lakini alipofika walimtaka akae kwenye 'Academy' yao ili ajifunze zaidi soka la kimataifa kwa mwaka mmoja bila kulipwa mshahara badala ya kufanya majaribio kama alivyoambiwa wakati anaenda. Jambo hilo lilikuwa gumu kwa straika huyo ndipo alipoamua kurejea kwao.

Mavugo ambaye atatambulishwa rasmi siku ya Simba 'Simba Day'  Agosti 8 amejiunga kambini na wenzake jioni ya leo baada ya timu hiyo kurejea kutoka Morogoro ilikoweka kambi ya takribani wiki mbili.

Post a Comment

 
Top