BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
STRAIKA mpya wa Simba, Laudit Mavugo raia wa Burundi ameangalia safu ya ushambuliajia ya Simba na kujitathimini kisha akatamka kwamba ni lazima aongeze jitihada kupata namba kwenye kikosi cha kwanza. 

Katika safu hiyo Mavugo atagombea namba na nyota wengine walio kwenye kikosi cha Joseph Omog ambao ni Ame Ally, Ibrahim Ajibu, Danny Lyanga na Fredric Blagnon ambaye ni raia wa Ivory Coast. 

Straika huyo ambaye amemaliza msimu uliopita akiwa na mabao 30 katika ligi ya Burundi huku akifunga mabao 62 kwa misimu miwili aliiambia BOIPLUS kuwa kwa siku alizofanya mazoezi amegunduankuna upinzani mkubwa ndani ya kikosi hicho. 

"Nimekuja kucheza na ndiyo kazi yangu, ni lazima niongeze jitihada ili kuhalikisha napata namba, sijaifahamu Simba kiundani ila kwa haraka haraka nimeona ni timu yenye ushindani," alisema Mavugo

Mavugo amesaini miaka miwili na amekuwa alisisitiza kwamba amekuja Simba kulipa deni kwani tangu achukuwe pesa yao ya usajili mwaka jana hawakumpeleka mahakamani kudai haki yao baada ya dili lake la kutua Msimbazi kushindikana.

Post a Comment

 
Top