BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu, Dar
BAADA ya kucheza soka kwa mafanikio makubwa mshambuliaji  mkongwe na nahodha wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi amestaafu rasmi soka na sasa anakuwa Meneja wa timu hiyo.

Licha ya Simba, Mgosi pia aliwahi kuichezea Mtibwa Sugar misimu tofauti kabla ya kutimkia DC Motemapembe ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo huku sifa yake kubwa ikiwa ni nidhamu na kujituma kwa timu zote alizozitumikia.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Manara amethibitisha hilo na kusema Mgosi ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaopigwa Jumapili ya Juma hili uwanja wa Taifa Dar es salaam dhidi ya URA ya Uganda.

Manara ameeleza kwamba aliyekuwa Meneja wa timu, Abbas Suleiman Ally anakuwa Mratibu wa timu (Team Coordinator) kuanzia leo na Nahodha mpya ni Jonas Gerald Mkude.


Aidha kiungo wa klabu hiyo, Peter
Mwalyanzi aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea timu ya Mbeya City FC, ametolewa kwa mkopo African Lyon iliyopanda kucheza ligi Kuu msimu huu wa 2015/16.

Inaelezwa mechi ya Simba na  URA itakuwa ya mwisho ambapo Agosti 20 wekundu hao watashuka dimbani kukipiga na Ndanda  wanakuchelechele katika uwanja wa Taifa.

Post a Comment

 
Top