BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
WAJUMBE wa kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga waliofutwa uanachama wamepeleka malalamiko yao kwa Shirikisho la Mpira miguu Tanzania (TFF) baada ya kukiukwa kwa katiba katika kufukuzwa kwao.

Wajumbe hao ni Ayoub Nyenzi, Hashimu Abdallah pamoja na Salum Mkemi ambaye aliupinga mkutano huo hadharani na kusema ulikiuka katiba ya klabu hiyo yenye historia kubwa ya soka katika nchi hii.

Katika barua kuonaonesha kuna ukiukwaji mkubwa uliotumika kuwafuta uanachama kinyume na katiba ya klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1935.

Katika mkutano mkuu wa dharura wa Yanga uliofanyika Agosti 6 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam uliazimia kuwafuta uanachama wajumbe hao kutokana na kuonekana wanaihujumu klabu hiyo na kusababisha kurudisha nyuma maendeleo ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuu.

Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas alisema wamepokea barua ya wajumbe hao Agosti 12 ambapo kamati husika itakaa kuipitia kabla ya kutoa ufafanuzi wa kinachotakiwa kufanyika baina ya pande zote mbili.

"Tumepokea barua hiyo ya malalamiko ambayo kamati husika itakaa kwa ajili ya kujadili kabla ya kutoa muelekeo ya kinachitakiwa kufanyika," alisema Lucas.

Post a Comment

 
Top