BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Mwetu
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 20 kitakachoingia kambini Agosti 28 kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kufuzu kombe la mataifa Afrika dhidi ya Nigeria.

Stars ambayo ilikuwa kundi G ambalo Misri wamekata tiketi ya kucheza michuano ya AFCON itakayofanyika nchini Gabon mwakani kitashuka dimbani Septemba 3 kwa mchezo wa kulinda heshima.

kikosi kamili, Makipa Deogratius Munishi 'Dida' na Aishi Manula.

Mabeki ni Mwinyi Hajji,Andrew Vicent, Kelvin Yondani, David Mwantika, Mohamed Hussein na Shomari Kapombe.

Viungo ni Himid Mao,Muzamir  Yassin, Farid Musa, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Jamal Mnyate Juma Mahadhi na Simon Msuva.

Washambuliaji ni Mbwana Samatta,Ibrahim Ajib, na John Bocco.

Post a Comment

 
Top