BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa kesho anatarajiwa kutangaza kikosi ambacho atakiandaa maalumu kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Nigeria 'Super Eagles' utakaopigwa Septemba 3.

Mkwasa amesema  anatarajia kuita wachezaji 20 ambao atasafiri nao kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo huo wa kukamilisha ratiba baada ya kutokuwa na nafasi tena ya kusonga mbele katika michuano ya mataifa barani Afrika ambapo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Gabon .

“Kutakuwa na mabadiliko kidogo katika kikosi nitakachotangaza kesho. Kwanza watakuwa wachezaji 20 badala ya 24, pili wachezaji ambao nitawachukua ni tofauti tofauti baada ya wengine kuwa  majeruhi kwa sasa” alisema Mkwasa.

Katika kundi hilo la G Misri imeshakata tiketi ya kucheza Fainali hizo  mwakani huku Tanzania na Nigeria wakiwa hawana nafasi tena baada ya Chad kujitoa mwishoni kutokana na ukata.

Tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Nigeria (NFA), limesogeza mbele kwa siku moja mchezo huo ambako sasa utafanyika Septemba 3, badala ya 2 kama iliyotangazwa awali.

Post a Comment

 
Top