BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Dar
MFANYABIASHARA Mohamed Dewji 'Mo' ambaye ni mwanachama pekee wa Simba aliyetangaza nia ya kuwekeza klabuni hapo, leo hii ametoa kiasi cha Sh 100 Milioni kama mchango wake kwenye usajili.

Mo alimkabidhi Rais wa Simba Evance Aveva hundi katika mkutano uliomalizika hivi punde ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa siku kadhaa zilizopita alipozungumza na waandishi wa habari.

Akizungumza katika mkutano huo Aveva alimshukuru Mo na kuwasihi wanachama wengine kuchangia usajili huo kwavile jumla ya pesa inayohitajika ni Sh 420 Milioni.

"Tunamshukuru sana Mo kwa kutimiza ahadi yake, hapa sasa tunaweza kutembea vifua  mbele kwavile kwa pesa hii tunaweza kukamilisha usajili wa straika Fredrick Blagnon ambao utatugharimu zaidi ya Sh 100 Milioni," alisema Aveva.

Kwa upande wake Mo alisema "Nilitaka mchakato huu ukamilike miezi mitatu au minne iliyopita ili tutume maskauti wanne au watano wazunguke kutafuta wachezaji bora Afrika.

"Pesa hii nimeitoa kwa mapenzi yangu tu kama nilivyoahidi, ni mapenzi yangu tu kwa klabu hii ya Simba," alisema Mo.

Aidha Mo aliomba mchakato wa mabadiliko ufanyike kwa haraka ili angalau ukamilike ndani ya miezi mitatu.

Post a Comment

 
Top