BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

BENKI ya NMB imetoa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kudhamini mashindano ya Rock City Marathon yatakayofanyika jijini Mwanza wikiendi ijayo.

Mbio zikazoshindaniwa ni kilomita 21,5,4 pamoja 2 kwa ajili ya watoto na watu wenye ulemavu wa ngozi  (albino).

Kaimu Ofisa mkuu wa wateja binafsi  wa NMB Boma Raballa amewashukuru waandaji wa mashindano hayo kampuni ya Capital Plus International kwa kutambua kuwa benki hiyo inaweza kushiriki kufanikisha jambo hilo.

Raballa alisema pia mwaka huu NMB wametenga shilingi bilioni moja kwa ajili ya kusaidia shughuli mbali mbali za kijamii zikiwemo na michezo.

"Tunawashukuru Capital Plus kwa kutambua kuwa tunaweza kushiriki kusaidia Rock City Marathon kufanyika" alisema Raballa.

Kwa upande wake Mratibu kutoka Kampuni ya Capital Plus Mathew Kasonta alisema mashindano hayo yalianza mwaka 2009 na mpaka sasa yamekuwa kuwa kivutio kwa watu wengi kutoka kanda ya ziwa.

Pia Kasonta amewataka wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa ya Jirani kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kwenye ofisi za michezo za wilaya zote mikoa ya Mwanza,Geita, Simiyu pamoja na Shinyanga.

Post a Comment

 
Top