BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

NYOTA sita wa kikosi cha Yanga wanatajiwa kukosa mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya African Lyon utakaopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kutokana na matatizo mbali mbali.

Mabingwa hao watetezi walishindwa kucheza mchezo wao wa kwanza wiki iliyopita baada ya kuwa na mechi ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe na kupoteza kwa mabao 3-1 mjini Lubumbashi.

Wachezaji wataokosekana kwenye mchezo huo ni Kelvin Yondani (Matatizo ya kifamilia), Juma Abdu (Msuli), Obrey Chirwa (Goti), Nadir Haroub (Nyonga),Malimi Busungu (matatizo ya kifamilia), Gofrey Mwashiuya (Goti).

Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga na wa pili kwa African Lyon ambao wana pointi 1 baada ya kulazimisha suluhu na Azam FC katika mchezo wao wa kwanza kwenye uwanja wa Azam Complex.


Yanga wamepania kuibuka na ushindi katika mchezo huu ili kurejesha matumaini ya kutetea ubingwa wao waliochukua kwa miaka miwili mfululizo.

Post a Comment

 
Top