BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
BAADA ya kuonyesha kiwango bora katika mchezo wake wa kwanza kuitumikia Simba, mashabiki wa Simba wanatarajia kujithibitishia ubora wa straika huyo katika mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya URA ya Uganda utakaopigwa jumapili hii kwenye dimba la Taifa.

Taarifa ambazo BOIPLUS imezinyaka kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema Simba imekamilisha taratibu zote za kucheza mechi ya kirafiki na watoza ushuru hao wa Uganda ambao wataanza kupepetana na wenyeji wao Azam FC kabla ya kuwavaa wana wa Msimbazi.

Kiongozi mmoja wa Simba alisema mchezo huo ni kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu huku pia ikiwa ni nafasi nzuri kwa kocha na mashabiki wa Simba kutazama uwezo wa wachezaji wao wapya akiwemo Mrundi aliyezikonga ghafla nyoyo zao, Laudit Mavugo.

"Ni kweli jumalipi hii tutakipiga na URA, Wanasimba waje kwa wingi uwanja wa Taifa waone picha kamili la Mavugo, ile juzi ilikuwa trela tu," alisema kiongozi huyo kwa majigambo.

Viingilio katika mchezo huo majira ya saa 10 alasiri vitakuwa kama ifuatavyo;
VIP A - 20,000
VIP B - 15,000
Na viti vingine vyote vinavyobaki ni 5,000. 

Post a Comment

 
Top