BOIPLUS SPORTS BLOG

Mpigapicha Wetu
Beki Kelvin Yondan anatarajiwa kuongoza safu ya ulinzi ya Yanga katika mchezo wa kesho dhidi ya Mo Bejaia

Kwenye mashambulizi, Yanga wamekuwa wakijivunia zaidi mawinga. Katika mchezo wa kesho Simon Msuva (pichani) na Deus Kaseke watakuwa na jukumu la kuwalisha mipira Amissi Tambwe na Obrey Chirwa

Ili safu ya ulinzi isipate wakati mgumu, timu inahitaji viungo imara. Pichani ni kiungo Thaban Kamusoko (kushoto) na kiraka Mbuyu Twite. Ubora wao kati mchezo wa kesho utakuwa wenye manufaa makubwa kwa timu

Kutoka kushoto ni Vicent Bossou, Kaseke, Haruna Niyonzima, Benno Kakolanya, Oscar Joshua, Twite, Tambwe na Pato Ngonyani Kama Yanga itashinda kesho, itakuwa imeamsha tena matumaini ya kufuzu kwa nusu fainali ya michuano hiyo ya kombe la Shirikisho

 Kocha Hans Van Pluijm akimsikiliza kipa Ally Mustapha 'Barthez'
Post a Comment

 
Top