BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Bunju
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Simba leo walitembelea mradi wa ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo uliopo Bunju

Rais Evans Aveva katikati akisalimiana na mwanachama mkongwe wa timu hiyo Bi. Hindu. Wengine kutoka kushoto ni mjumbe Said Tully, Mzee Hassan Dalali na Iddy Kajuna (kulia)

Mzee Dalali katikati akipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa matawi na wanachama waliotembelea Bunju leo

Wapenzi wa Simba walioongozana na viongozi kukagua mradi wa ujenzi wa uwanja huo

Mkurugenzi wa kampuni inayosimamia masuala ya masoko ya klabu ya Simba (EAG), Imani Kajula akimweleza jambo Aveva huku katibu mkuu Patrick Kahemele akisikiliza kwa makini

Hawa ndio wanaohakikisha eneo la Simba linakuwa salama wakati wote. Walinzi hawa walianza kazi tangu eneo hilo liliponunuliwa

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Ally Suru na Tully wakibadilishana mawazo

Huu ndio uwanja ambao ulifyekwa kwa mapanga na wanasimba wakati wa Uongozi wa Ismail Rage. Mradi mpya unafanyika eneo jingine lililo jirani na uwanja huo ambao ni maarufu kwa jina la 'Uwanja wa Rage'

Hapa ndipo mradi mpya wa ujenzi unapofanyika. Kwa mbali wanaonekana viongozi na wanachama wa klabu hiyo wakizunguka kukagua

Aveva akizungumza na wanachama walioshiriki ziara hiyo mara baada ya zoezi kukamilika

Aveva akimweleza jambo mwandishi wa BOIPLUS kuhusu mipango ya ujenzi wa uwanja huo

Baada ya zoezi kukamilika, Bi. Hindu aliamua kufanya dua. Tembelea akaunti yetu ya Youtube kwa jina la BOIPLUS TV utazame alichokiomba.

Post a Comment

 
Top