BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
RATIBA ya nusu fainali ya Michuano ya  klabu Bingwa barani Afrika imetoka ambapo  Zamaleki ya Misri itacheza na Wydad Casablanca ya Morocco huku Zesco ya Zambia ikimenyana na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini. 

Kwa upande wa kombe la shirikisho TP Mazembe itamenyana na Etoile du Sahel ya Tunisia, huku MO Bejaia ya Algeria wakiumana uso kwa uso na waarabu wenzao wa FUS Rabat ya Morocco.

Atakayeibuka mshindi kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika atanyakua kitita cha dola 1.5 milioni pamoja na kupata tiketi ya kushiriki klabu bingwa ya dunia.

Ratiba ya Klabu Bingwa:

Sept 16-18, 2016
Zamalek (Misri) Vs Wydad Athletic Club (Morocco)

Zesco (Zambia) Vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)

Ratiba ya Kombe la Shirikisho:

Sept 23-25, 2016
TP Mazembe (DRC) Vs Etoile du Sahel (Tunisia)

MO Bejaia (Algeria) Vs FUS Rabat (Morocco)

Post a Comment

 
Top