BOIPLUS SPORTS BLOG

GENK, Ubelgiji
STRAIKA na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta ameiwezesha klabu yake ya KRC Genk kufuzu kwa hatua ya makundi ya ligi ya Europa baada kuwatoa Lokomotiva Zagreb kwa jumla ya mabao 4-2.

Samatta aliipatia Genk bao la kuongoza katika dakika ya pili tu ya mchezo kabla swahiba wake Leon Bailey hajapigilia msumari wa pili dakika ya 50 na kuifanya timu hiyo iibuke na ushindi wa mabao 2-0.

Katika mchezo wa awali alifunga bao moja katika sare ya mabao 2-2 nchini Croatia na sasa wanasubiri kujua watapangiwa kundi gani ikiwa ni rekodi nyingine kwa mtanzania huyo.

Kocha wa Genk Peter Maes alimtoa Samatta katika dakika ya 80 na nafasi yake kuchukuliwa na Nikos Karelis.Post a Comment

 
Top