BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
WAKATI mfanyabiashara kipenzi cha wanamsimbazi Mohamed Dewji 'Mo' akiwasilisha barua ya kutangaza azma ya kuwekeza Simba, kikosi cha timu hiyo kimeibuka na ushindi mkubwa wa mabao 5-0 dhidi ya Burkinafaso ya Morogoro katika mchezo wa kujipima ubavu uliofanyika uwanja wa Jamhuri jioni ya leo.

Magoli ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajib aliyefunga mawili, mengine yakifungwa na Musa Ndusha, Shiza Kichuya pamoja na Saidi Ndemla.

Wekundu hao wanaonelewa na kocha Mcameroon Joseph Omog wamekuwa na matokeo mazuri katika mechi za kirafiki baada ya wiki iliyopita kuibugiza Polisi Morogoro magoli 6-0 kabla hawajashinda kwa mabao 2-0 dhidi ya kombaini ya Moro.

Kikosi hicho kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi Interclub ya Angola inayonolewa na kocha Dravko Logarusic katika mchezo wa kuadhimisha Simba Day Agosti 8.

Post a Comment

 
Top