BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi & Ally Shatry, Dar
 Kiungo wa Simba Shiza Kichuya kushoto akitafuta mbinu za kuwatoka walinzi wa JKT Ruvu

 "Leo hakuna njia hapa"......Salim Gila akimdhibiti winga wa Simba Jamal Mnyate

 Beki aliyeziba nafasi ya Hamad Juma aliyeumia, Malika Ndeule alionyesha kandanda safi na kuwaonyesha wanasimba kuwa hawakukosea kumuongeza dakika za mwishoni

 Nahodha wa Ruvu Michael Aidan akiwa 'mguu sawa' kuhakikisha Laudit Mavugo haleti madhara langoni mwao

 Walichofanikiwa walinzi wa Ruvu jana ni kuhakikisha washambuliaji wa Simba hawapati utulivu wanapolifikia lango lao

 Krosi zilizopigwa na Kichuya hazikuweza kuzaa matunda kwavile nyingi ziliishia vichwani mwa walinzi wa Ruvu au kupotezwa na washambuliaji wa Simba

 Straika Fredrick Blagnon alipata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza, bado utulivu na maelewano baina ya washambuliaji yalikuwa tatizo kwa Simba kupata mabao

Wachezaji wa akiba Mwinyi Kazimoto, Juuko Murshid, Mohamed Ibrahim na Abdi Banda

"Dakika zinakwenda wazee"......maofisa wa benchi la ufundi la Simba wakitafakari cha kufanya kwenye dakika za mwisho  za mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya 0-0

Post a Comment

 
Top