BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu  Rajabu, Dar
KIKOSI cha Simba kinaingia kambini hii leo kuivutia kasi JKT RUVU katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa Jumamosi Agosti 27.

Katika mchezo uliopita Simba iliibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Ndanda na kuonesha kandanda safi ambalo liliwavutia mashabiki waliohudhuria.

Kocha msaidizi wa Wekundu hao Jackson Mayanja ameiambia BOIPLUS kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo huo ili kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa.

"Tunaingia kambini leo kwa ajili ya mchezo wetu wa Jumamosi ambao tumejipanga kushinda, Wachezaji pia wanalijua hilo na wamesema watalitekeleza" alisema Mayanja.

Aidha Mayanja ameusifu uongozi wa Wekundu hao kwa kuwezesha kusajili wachezaji wazuri ambao wanaweza kurejesha hadhi ya klabu hiyo iliyopotea kwa miaka minne sasa.

Mayanja alisema Simba haikufanya vizuri katika msimu uliopita kutoka na kutokuwa na  kikosi kipana kwenye nafasi mbali mbali ndiyo maana wakashindwa kumaliza ligi vizuri lakini sasa wana wachezaji bora watakaoleta neema Msimbazi.

Katika mchezo wao awali dhidi ya Ndanda magoli yao yalifungwa na Laudit Mavugo, Fredrick Blagnon na Shiza Kichuya.

Post a Comment

 
Top