BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Dar
TIMU ya Taifa ya mpira wa Ufukweni ya Tanzania imekubali kichapo cha mabao 7-3 toka kwa Ivory Coast katika mchezo wa kwanza hatua ya awali ya kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika Soka la ufweni uliofanyika kwenye uwanja maalum Karume jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi na mashabiki wengi wenyeji walionekana kuzidiwa ujanja na wageni kutokana na uzoefu waliokuwa nao.

Mabao ya wageni yalifungwa na Kablan Assouan Bile aliyefunga matano huku mawili yakifungwa na Aka Kablan Frederic.

Kwa upande wa wenyeji mabao yao yalifungwa na nahodha Ally Rabi aliyefunga mawili huku jingine likifungwa na Samwel Sarungi.

Mchezo huo unachezwa kwa dakika 36 huku wachezaji watano watano kila upande wakianza kabla ya kufanya mabadiliko.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Septemba 18 mjini Abjan Ivory Coast huku Tanzania wakitakiwa kushinda mabao 4-0 ili kufuzu kwa hatua inayofuata.

Post a Comment

 
Top