BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
STRAIKA Laudit Mavugo aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na wekundu wa Msimbazi Simba ametua uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere usiku huu na kupokelewa na Makamu wa Rais wa klabu hiyo Geoffrey Nyange 'Kaburu' pamoja na mashabiki.

Mavugo raia wa Burundi alikwenda nchini Ufaransa kufanya majaribio lakini taarifa zinasema ameshindwa majaribio hayo na kabla hajatua nchini alionekana jijini Kigali na haikufahamika alifuata nini.

Inafahamika kuwa Mavugo ambaye ni tegemeo katika kikosi cha Vital'O alishapokea sehemu ya pesa yake ya usajili ambayo alikubaliana na wekundu hao mwaka jana na ujio wake ni wazi utakuwa kwa lengo la kukamilisha tu usajili huo.

Tayari Simba kupitia kwa Rais wake Evance Aveva ilishatangaza kuridhishwa na kiwango cha mshambuliaji Fredrick Blagnon raia wa Ivory Coast ambaye yupo kambini mjini Morogoro huku wakiweka wazi kuwa watatumia kiasi cha Sh 100 milioni zilizotolewa na Mohamed Dewji 'Mo' kumaliza usajili huo.

Post a Comment

 
Top